ALICHOKISEMA NYANDU TOZI KUHUSU MR BLUE KUTUMIA MADAWA YA KULEVYA

Taarifa zilizokuwa zikisika Chini kwa chini mtaani ni kuwa Msanii Mr Blue kwa sasa anatumia Madawa  ya Kulevya, Ambayo yanamsababisha Kupunguza Ufanisi wake wa Kufanya Kazi na Hata Kubadilisha Muonekano wake na Kuwa tofauti kabisa na Alivyokuwa Mwanzo.

Kupitia Kipindi cha TV Nyandu Tozi alikuwa akizindua Video ya wimbo wake Mpya Ambao unajulikana kwa jina la MAMBO MENGINE BAADAE ambao amemshirikisha Mr Blue katika Chorus.
Kama ni Mfatiliaji wa Muziki Basi utakua unajua kuwa Mr Blue na Nyandu Tozi ni Marafiki wa Karibu sana , Kutokana na urafiki na Ukaribu  waliokuwanao basi ni rahi kujua jambo lolote ambalo linaendelea kwa Rafiki yake, Na Nyandu Tozi alipo ulizwa kuhusu Mr Blue kutumia Madawa ya Kulevya Alijibu Hivi...   

"Unajua Mafans wanashindwa Kutofautisha, kwa sasa Mr Blue anafanya maisha yake na ana Mtoto  so kwa sasa yeye ni Baba hawezi kufanya Mambo kama aliyokuwa akifanya Zamani, Yule ni mwangu na Vile vitu hatumii ni mfumo tu wa maisha ameamua kubadilika"

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment