Nisher ndiye muongozaji bora zaidi wa video Tanzania au ni mmoja kati yao? Mwenyewe ajibu swali hili kwa mtazamo wake

‘Nisher Entertainment au Directed by Nisher’, haya ni maandishi ambayo utakuwa umeyaona kwenye video bora za Tanzania zilizoweza kuvuka mipaka na kuoneshwa na vituo vikubwa vya runinga duniani kama Channel O.
Muongozaji huyu ambaye ameongeza ubora na kuongeza changamoto zaidi kwenye kiwanda cha video za muziki Tanzania akiwa ameongoza video zilizoshika attention ya watu wengi kama ‘Jikubali’ ya Ben Pol, ‘Kijukuu’ na hivi karibuni kuzua gumzo na ‘Nje ya Box ya Weusi’…kwa kuzitaja chache kati ya nyingi bora.
Mtaani kuna mengi yanaendelea kuhusu ujio na kazi za Nisher kwenye kiwanda hiki cha video nchini, huku Adam Juma wa Visual Lab akitajwa kuwa mtayarishaji wa kwanza kuziletea heshima kubwa video za muziki Tanzania kwa ubora wake, na wengine wakiungana na maoni yaliyotolewa na mhariri mkuu wa mtandao wa Bongo5 yaliyomtaja Nisher kama mtu anayeweza kuziba gap la Adam Juma endapo akiacha kufanya video za muziki kama alivyoeleza hapo awali.
Mjadala kuhusu nani ni muongozaji bora zaidi wa video kwa sasa Tanzania unaendelea kimyakimya kati ya wadau wa muziki, na kuna wakati maelezo ya muongozaji huyo kwenye mtandao wa kijamii yaliwahi kuleta utata na kuchukuliwa kuwa yeye anajiona kama bora zaidi kwa sasa.
Huenda watu hawakuelewa vizuri ama walikuwa sahihi kwa kile walichokitafsiri kutoka kwenye maandishi ya Nisher.
HOT SHOW ya HIGHLANDS  Fm imemtafuta muongozaji huyo ili kupata maoni yake ama majibu yake binafsi juu ya swali hilo linalozua mjadala kwa wadau wa muziki.
“Mimi nawaachia watu zaidi.” Amesema Nisher. “Mimi career yangu ama kazi yangu ninayoifanya iko fan based zaidi. yaani mimi hapa nasikiliza watu kile wanachokisema kuhusu mimi.
“Wao wakiona kwamba mimi ndio the best na hakuna mwingine, basi sawa, wakiona mimi ni one among the best basi sawa. Kwa sababu wao toka mwanzo ndio wamenipa hii chance, wao toka mwanzo ndio wameinikubali wameniweka hapo. Media houses mbalimbali kama nyie na wengineo. Nyie ndio mmenifanya mimi kuwa hivi na nyie ndio mnanijaji kuwa mimi ndio the best hakuna mwingine au mimi ni one among the best.” Nisher ameiambia HOT SHOW
Majibu ya Nisher yanaurudisha mjadala huo kwa mashabiki wenyewe na media houses kwa ujumla. Kazi ndizo zitakazoendelea kuongea.
Hivi karibuni Nisher aliweka wazi kuwa baada ya video ya ‘Nje ya Box’ ya Weusi, video nyingine zitakazooneshwa hivi karibuni kwenye kituo cha runinga cha Channel O ni Kijukuu ya Young Dee, Mama Yeyo ya G.Nako na Baby ya Mirror.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment