Fid Q aitaja 'Machozi Jasho na Damu' ya Profesa Jay kama albam bora ya karne


Rapper toka Rock City Mwanza, Fareed Kubanda aka Fid Q ama Ngosha The Swag Don ameipa nyota zote albam ya Profesa Jay ya mwaka 2001 ‘Machozi Jasho na Damu’, na kuitaja kama albam bora zaidi ya karne.
Tajiri huyo wa mashairi na flow ametweet ujumbe huo wakati akijibu tweet ya Oscar Maboko aliyoeleza kuwa albam hiyo iliuza nakala milioni kadhaa lakini iliathiriwa na wizi za kazi wasanii.
"#MachoziJashoNaDamu is an indisputable/classic/dope/great&prolly the best album of the 1st century! #PROFJ @OscarMaboko @africanhiphop." Ametweet Fid Q.
Katika hatua nyingine, mdau huyo wa muziki, Oscar Maboko alieleza kuwa anaamini hata albam ya kwanza ya Sugu enzi hizo anaitwa 2 Proud iliathiriwa kimauzo na kanda za kurekodi kwenye Fm Radio zilizokuwa zinauzwa mtaani na kwamba karibia kila kijana aliyekuwa na radio cassette alinunua nakala hizo.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment