KWELI MR.NICE SIKIO LA KUFA:BAADA YA KUHAMIA KENYA AENDELEZA TABIA ZILIZOMFANYA AFILISIKE BONGO


Hakika  Tabia  ni  ngozi....
Ni vigumu  kuamini, lakini  ukweli  ni  kwamba Mr.Nice  ameirudia  tena  ile  tabia  yake  ya Ukicheche  na  kuwapanga  wanawake  mithiri  ya vyombo  kabatini  iliyomfanya  afulie  na  hatimaye  kuwa  omba omba.....

Taarifa  toka  nchini Kenya  ambako kwa  sasa  msanii huyo  yupo huko  ni  kwamba, Mr. Nice   kwa  sasa   alala  baa  akiwa  amezungukwa  na  warembo  kadhaa wanaojua  kuzitumia  pesa...!!!!

Nice amekuwa  akionekana  katika  mitaa kadhaa  ya jiji  la Nairobi akiwa  na  "mabodigadi wa kike" ambao  amejitolea  kuwadhamini   LUNCH, DINNER na MATANUZI  mengine...

Hongera  kwa  moyo wa upendo Mr. Nice...Tunajua  kwamba  si  vizuri  tukakupangia  matumizi  ya pesa  yako, lakini  tunakuonea  huruma  maana  historia  yako  tunaijua tangu  enzi  zile  ulipokuwa   ukitamba  na  nyimbo  zako  za "Kikulacho  ki  nguoni  mwako"   kabla  ya  kufilisiwa  na  akina  dada  wa  mjini....
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment