camera.
Katika kipindi hicho cha jana jumapili (may 12) wameonekana wasanii wa THT Linah na Barnaba ambao walieleza kuwa watakuwepo katika show ya miaka 13 ya Lady Jay Dee kumsapoti, na kwa pamoja wasanii hao walitaja kiingilio na kwamba watu wahudhurie ili kumsapoti Jide ambae ni dada yao na mama yao mpendwa.
Lakini Barnaba na Linah hivi karibuni walikana kuwa hawatahudhuria katika show ya Jide ya May 31 itakayofanyika Nyumbani Lounge licha ya kuwa katika matangazo, na sababu ikiwa kutofikia maafikiano ya kibiashara na uongozi wa wasanii hao. Na kwamba hakuna makubalino yeyote yaliyofikiwa kati yao, lakini pia walisema hawana ugomvi na Lady Jay Dee.
Kwa upande wa Jide yeye anasema alishalipia advance kwa ajili ya kufanya kazi na wasanii hao wa THT na ndiyo sababu wako kwenye posters. Na kwamba anajua watakuwa wamekatazwa na maboss wao.
Hapa kuna mkanganyiko wa maelezo na ni vigumu kufahamu nini kiko nyuma ya pazia, makubaliano ya awali hadi kufikia hatua ya kushoot kipande hicho cha tangazo. Na kwa nini wasanii hao wanakataa kata kata kuwa na makubaliano na Jide kuhudhuria show yake.
Ni yapi maoni yako kuhusu hiki kinachoendelea?
0 comments:
Post a Comment