MWANAMUZIKI nyota wa Bongo Fleva, Judith Wambura Mbibo ‘Lady Jaydee’ Leo
(Jumatatu) anatarajia kuripoti Mahakama ya Kinondoni kufuatia taarifa
alizofikishiwa Meneja na mume wa msanii huyo, Gadna G Habash ‘Captain’.
Gadna alisema ni kweli wamepata taarifa za kutaarifiwa Lady Jaydee
kufika Mahakama ya Kinondoni, leo (Jumatatu) Mei 13, mwaka huu.
“Ni kweli tumepata wito na Mahakama ya Kinondoni, hii ni baada ya kufika
watu ambao walijielezea kuwa wanatoka Mahakama hiyo jana na kuleta
barua ya kumkabidhi Lady Jaydee mwenyewe japo hawakumkuta” alisema
Gadna.
Katika ukurasa wa Twitter wa Lady Jaydee saa tatu zilizopita aliandika
hivi "Sumu ya teja Ukonga, Keko, Segerea. Kesho Mahakamani kizibiti
ubaoniii eeeh aaah!" wakati siku ya Ijumaa katika ukurasa wake wa
Facebook aliandika hivi:
"Ratiba ya usiku wa leo ni MACHOZI BAND kama kawaida, ila ratiba ya
Jumatatu natakiwa Mahakama ya Kinondoni... Taarifa zaidi zitafuata
nikijua kinachoendelea... Ila kwa leo mje tuburudike Nyumbani Lounge mpk
asubuhi."
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment