Rapper kutoka mji kasoro bahari
[MOROGORO],
AFANDE SELE "THE KING"ametoa shukrani zake kwa Mbunge wa
KIGOMA, TANZANIA Mh. Zitto Kabwekupelekea msaada aliompatia ...
AFANDE ambae hivi sasa anatamba na ngoma yake ya DINI TUMELETEWAambayo amempa shavu msanii Belle 9 mapema masaa machache yaiyopita kupitia ukurasa wake wa Facebook ameonekana akitoa shukrani zake za dhati kwa Mh. Zitto Kabwe kwa kuweza kugharamia gharama zote zitakazotumika kwenye utengenezaji wa video ya ngoma yake hiyo ...
Hiki ndicho alichokiandika kupitia ukurasa wake huo, soma hapa chini ...
Afande Sele "The King"Lengo la hii kazi yangu mpya DINI TUMELETEWA ni kumrudisha mwafrika kwenye uafrika wake ambao msingi wake ni UMOJA, USHIRIKIANO NA UPENDO. Ambao kwa siku za hivi karibuni tumeshuhudia ukitoweka. Tumeona mapigano/mauaji ya itikadi za kidini wenyewe kwa wenyewe, pia kuelezea uhuru wa kuabudu kwa imani yoyote bila kuvunja sheria za Taifa letu. Kwa mtu yoyote makini mwenye mapenzi mema kwa Taifa letu na AFRIKA hawezi kupingana na hilo, kwa kutambua hilo MH; ZITTO ZUBERI KABWE(ZZB) kajitolea kugharamia gharama zote kwa ajili ya kufanikisha vidio bora kabisa ya wimbo huu, hii ni kazi yetu wote mimi na wewe, tunasema asante sana kwa Mh; Zitto. AMANI NA UPENDO KWANZA"
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment