50 Cent amuomba radhi kijana mlemavu wa akili aliyemdhania ni teja.

Rapa 50 Cent ameomba radhi familia ya kijana mlemavu wa akili kwa kupost video ya kijana huyu akiwa kazini na kusema ametumia kilevi flani huku akifanya kazi kwenye uwanja wa ndege nchini Marekani.
50 Cent alipondwa vikali na mashabiki wake kwa kitendo hicho alichomfanyia kijana huyu huku familia yake ikitaka awaombe radhi uso kwa uso na kulipa faini ya dola milioni moja.
0504-50cent-letter-rip-1
50 Cent ameomba radhi kwa kuandika barua kumuomba msamaha kijana huyo aitwaye Andrew Farrell.
Na sasa familia yake imemtaka 50 cent alipe dola 100,000 kwa taasisi ya Autism Speaks, Mchango huo ni mdogo zaidi ukilinganisha na dola milioni 1 ambazo baba wa kambo wa Andrew alitaka walipwe
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment