Chanzo cha kifo cha baba mzazi wa Dullysykes na taarifa ya maziko.

Marehemu Mzee Abby Sykes ambaye ni Baba
mzazi wa mwimbaji wa Bongo Fleva Prince
Dullysykes, alifariki saa 8 mchana February
15 2015 akiwa hospitali ya taifa Muhimbili
kwa ajili ya kupatiwa matibabu.
Dullysykes amelitolea ufafanuzi suala hilo
ikiwa ni pamoja na kuelezea kitu
kilichosababisha umauti wa baba yake
ambapo anasema
"Mzee alikua ana vidonda katika miguu na
ndiyo chanzo kikubwa, sumu ikasambaa
ikasababisha kifo chake, vidonda
vilishindwa kupona kwa ajili ya moshi wa
sigara ila zaidi hakuwa na tatizo jingine
lolote manake baba yangu alikua strong"
‘Alianza kuugua vidonda miezi minne
iliyopita, miezi miwili alikua anavumilia tu
lakini miezi miwili ya mwishoni ndiyo
vilizidi kumsumbua, mazishi tunategemea
kuyafanya February 16 2015 saa kumi jioni
kwenye makaburi ya Kisutu lakini safari ya
kwenda msikitini tutaanza saa 7 mchana"–
Dully.
Mzee Sykes alizaliwa mwaka 1952.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment