Dr Dre ashangilia baada ya Apple kuinunua kampuni yake "Beats Electronics" kwa dolla bilioni 3.2, adai yeye ni msanii bilioea wa hip hop

WWW.STREETCONSCIOUS.BLOGSPOT.COM
Dr Dre Ameifuta record ya Forbes iliyowekwa na P Diddy mwaka huu. Kama unakumbuka Forbes ilitoa list ya wasanii wa hiphop watano walio na mkwanja, ambapo Dre alikuwa nafasi ya pili kwa kuwa na dola milioni 550 ambapo Didiy alikuwa anaongoza kwa kuwa na dola milioni 700.
Kwa mujibu wa habari zilizotoka leo hii, kampuni ya Apple inampango wa kuinunua kampuni ya Dre Beats Electronics kwa dola bilioni 3.2. Kampuni hiyo ilianzishwa na Dre pamoja na Jimmy mwaka 2008 kwa kutengeneza vifaa vya sauti kama headphones, speaker za magari pamoja na mtandao wa ku stream muziki.
Baada ya maneno kusambaa kuwa kampuni ya Apple iko mwishoni kukamilisha mkataba huo, Dre alienda studio akiwa na Tyrese, F Gary Gray (Big time movie director) na baadhi ya washkaji nakusherehekea kwa chupa za Champagne, Heineken na Henennessy. 
katika video waliji-record Dre ameonekana akiangalia camera na kusema "Bilionea wa kwanza katika game ya hip hop, kutoka west coast.
huku Tyrese akisema "oooh sh""t list ya Forbes imebadilika
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment