Mtayarishaji wa muziki ambaye pia mwimbaji, Lucci Tsere amepanga kurudi studio na kupika midundo itakayozaa ngoma kali kama zile alizofanya na Cpwaa na Black Rhino, kazi ambazo amedai zitawapeleka level ya kimataifa wasanii atakaofanya nao kazi.
Akiongea na HIGHLANDS FM kupitia HOT SHOW , Lucci amesema atawafanyia kazi bure wasanii atakaowachagua, lakini kazi hizo atazisimamia yeye.
“Kwa hiyo mpango wangu nitajaribu kukusanya wasanii niwape kazi za bure lakini nazisimamia mimi mwenyewe kama zile zilizowahi kufanya kwa level ya kimataifa, kazi ya CPwaa na Black Rhino. Kwa hiyo huo ndio mpango wangu mkubwa sana.”Producer Lucci ameeleza.
Hata hivyo, producer huyo bado haridhiki na kupigwa kwa nyimbo za baadhi ya wasanii wa Tanzania kwenye vituo vikubwa vya runinga kuwa ndio kitu kizuri cha kushangilia.
“Mwaka huu nimepanga kubadili mfumo mzima wa game wa Tanzania kwa sababu bado tunateseka, hata kama video inachezwa Trace au Channel O sio jambo la kushangilia sana,kwa mfano Trace wanacheza video za A.Y na Diamond,Je, Tanzania kama Tanzania tunanufaika na kitu gani hapo?.” Lucci amehoji

0 comments:
Post a Comment