Godzilla kuachia wimbo mpya wiki ijayo, unaitwa 'You and I', sasa anasambaza mixtape yake 'Zillax' kwa njia ya mtandao

Godzilla kuachia wimbo mpya wiki ijayo, unaitwa

Baada ya kuachia ‘Tungi’ siku kadhaa zilizopita, rapper Godzilla aka King Zilla wa Salasala, anatarajia kuachia wimbo wake mpya alioupa jina la You and I, wimbo ambao amemshirikisha producer wa MJ Record, Marco Chali.
Hata hivo, mashabiki wa Godzilla watamsikia mkali huyo wiki hii akiwa na Diamond Platinumz, kwenye wimbo walioshirikishwa na mdogo wake Marco Chali, Zachaa unaitwa ‘Mtoto wa Mama/What’s my Name.
“Kuna ngoma inakuja ambayo ni ya Zachaa ambayo iko kwenye mixtape yake, Zachaa amenishirikisha mimi na Diamond Platinum, ni wimbo wa Zachaa na ni production ya Marco Chali. Baada ya hiyo wiki inayofuatia ntatoa ya kwangu ambayo mimi nimemshirikisha Marco Chali, inaitwa You and I.” Godzilla ameiambia tovuti ya Times Fm.
Ameongeza kuwa mixtape yake ya Zillax inaenda vizuri na kwamba tayari nakala 200 za kwanza alizotoa zimekwisha, lakini hivi sasa inaweza kupatikana kwenye mtandao.
“Mixtape ya Zillax imetoka na copies 200 za kwanza ambazo nilikuwa nimezitengeneza ziliisha. Sasa hivi nimeamua system mpya kabla ya kugonga copy nyingine, zipo kwenye website ambayo nimeweka link yake kwenye page yangu ya Instagram, kwenye Facebook na kwenye Twitter, watu wanaweza kuingia wakadownload hiyo mixtape wataipata huko. Na naendelea na utaratibu mwingine ambao ntawafikia watu.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment