Msanii wa mpya wa kizazi cha sasa cha HIP HOP Kendrick Lamar huko marekani amesema inabidi apunguze kidogo ukali wa mistari yake kutokana na watu na baadhi ya wasanii wenzake kumtafsiri vibaya kwenye wimbo alioshirikishwa na Big Sean uitwao Control.
Kwenye Track hio kali ambayo Kendrick alikomaa vibaya katika vesi yake na kisha kuwataja rafiki zake ambao ni wasanii wa miondoko ya Hip Hop, wakina Drake, Asap Rocky, J. Cole na baadhi ya wasanii wengine kwa kusema kwamba anawapenda lakini atawamaliza wote kwenye gemu kiasi cha kwamba mashabiki wao hawata wasikia wasanii hao kutoa hata neno moja tena.
Lakini Msanii Drake alijibu na kusema kwamba Kendrick hawezi kumpoteza kwenye gemu na nikwamba japo marafiki lakini ukweli kwenye gemu lazima mashindano yawepo na sio kwamba kuna Bifu wala tatizo jingine, Its just an Ambition, hayo ndio maneno aliotoa Drake.

0 comments:
Post a Comment