Amber Rose aponda ushiriki wa Kanye West kwenye Remix ya 'Drunk in Love'? Adai wimbo mzuri umeharibiwa

Amber Rose aponda ushiriki wa Kanye West kwenye Remix ya


Mashabiki wa wimbo wa Beyonce, Drunk in Love aliyomshirikisha mumewe Jay Z, wanaweza kuwa waliifurahia pia Remix ya wimbo huo iliyoongezwa ladha ya shemeji yake Beyonce, Kanye West. Lakini ex-girlfriend wa Kanye West, Amber Rose anaweza kuwa hakuipenda kabisa hiyo.
Amber Rose, aliandika tweet baada ya kutambulishwa remix ya wimbo huo, tweet iliyosomeka wazi kuwa wimbo wake anaoupenda zaidi, kwa kiingereza ‘her favourite song’, umeharibiwa.
“F**k my fav song is ruined. Smh. Terrific.” Inasomeka tweet ya Amber Rose ya February 15.
Hata hivyo baada ya watu kuizungumzia, aliandika tena tweet nyingine akikanusha kuwa hakuwa anauongelea wimbo huo. Na kudai kuwa anaichukia twitter kwa kuwa yeye alikuwa anaongelea wimbo wa mumewe Wiz Khalifa ambao alimpa mtu mwingine.
“Just landed I was talking about my hubby’s song that he gave to someone else & I picked the one day “he” comes out with a song just my luck. I fu**ing hat twitter.” Aliandika. 
Katika verse ya Kanye West aliyoimba kwenye Remix ya Drunk in Love, anasikika akielezea maisha ya chumbani kati yake na mama mtoto wake  Kim Kardashian.
Mwaka 2012, Amber Rose aliliambia jarida la Star kuwa aliachana na Kanye West kwa kuwa alikuwa anam-cheat na Kim Kardashian, na kwamba Kim Kardashian alikuwa anamtumia picha Kanye halfu Kim alipozikamata alimwambia Kim aache kufanya hivyo, lakini hakumjibu hadi walipoachana kisha Kim Kardashian akachukua nafasi rasmi
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment