Janjaro ameiambia HOT SHOW kuwa anatarajia kuachia wimbo huo alioufanya ndani ya studio za B’Hitz chini ya producer Pancho Latino na kwamba humo ndani ameonesha upendo kwa Madee na Tundaman, pamoja na Boss wao Babu Tale, amewaomba wasahau ya kale kwa kuwa yeye sio Nabii.
Janjaro aliipa HOT SHOW ya HIGHLANDS Fm sehemu ya mashairi yaliyopo kwenye ngoma hiyo.
“Bado niko macho nasukuma gurudumu, nashukuru nikipatacho kinacover majukumu. Tusahau ya kale Tunda msalime Madee, mwambie Babu Tale Janjaro sio Nabii…”
Janjaro ameielezea kwa ufupi mistari hiyo, “vitu kama hivyo vinaleta upendo katika wimbo. Unajua kitu kama Tip Top ni watu ambao mimi wamenilea, kwa hiyo Janjaro sio nabii, hata glass hugongana…kunatokea matatizo lakini tusahau ya kale.”
Ameeleza kuwa hivi sasa uhusiano wake na Madee umeimarika na wanaongea vizuri. Amewashukuru watanzania kwa upendo wanaomuonesha.
0 comments:
Post a Comment