AZMA AFUNGUKA JUU YA ALBUM YAKE YA ATHMA(AZMA) ATTACK YENYE VIDEO TUPU

AZMA THE AFRICAN AMBASSADOR
Ni wasanii wachache wa Hip Hop Africa mashariki pengine na afrika nzima kwa ujumla waliowahi kutoa na kupeleka sokoni album zao zenye video tupu, uchache huo pengine unatokana na kutokuwa na mda wa kutosha kuandaa album yenye video tupu ama kutomudu gharama za kifedha kufanya video.
Azma a.k.a the African ambassador hit maker wa Kipimo cha penzi, Wanasuburi nife na Mungu inusuru Tanzania atakuwa msanii wa kwanza wa Hip Hop nchini Tanzania kutoa album yenye video tupu.
Akiongea na blog ya bongo Xclusives Azma amefunguka kuwa alipokuwa jijini mwanza mda mwingi aliutumia kufanya video za ngoma zake zitakazopatikana kwenye album yake mpya itakayotoka hivi karibuni.
AZMA, BOB RAY KATIKA, NA VIDEO QUEEN
“ Athma (Azma) attack ni shambulio la azma,  nimejaribu kuzugumza vitu vyenye ukweli ndani yake juu sanaa yetu na maisha yetu wa ujumla, watu wategemee vitu vikubwa kwenye hii album ya video yenye ngoma kumi na nane (18),  ni albam ya kwanza ya hip hop afrika mashariki ama afrika nzima kama sijakosea yenye video tupu, kuna wasanii wapo kwenye game kwa mda mrefu lakini hawana hata video tano (5) kwa hiyo this is a new attack”.
“msukumo wa kutoa album ya video ni kutokana na nature ya mauzo ya album yangu ya kwanza, wateja wangu ambao kila nilipokuwa nikipeleka album yangu ya love stories walikuwa wakiulizia video so niligundua nikitoa album ya kuona italeta impact, kingine ni huu ulimwengu wa digital, kuna sehemu zingine radio na tv za tanzania hazijafika huko… (nje ya nchi) so niliona nikitoa album ya video itaweza kuwafikia kiurahisi na on time”.
Kwa zaidi ya asilimia themanini (80%) album ya “Athma (Azma) Attack” video zimetengenezwa na Kinye media chini ya mwalim Kinye wa Saut na director Bob ray  ambae ni mdogo wake Kinye na baadhi ya video zimefanywa na directors tofauti tofauti, kwa upande wa audio kwa asilimia kubwa producer P. Mally wa Moss Records ndio kahusika, na baadhi ya prodcers kama  Double na D classic wamechangia pia. Ngoma zitakazopatikana kwenye hii album ni Mungu inusuru Tanzania, wanasubiri nife, mama, Azma Attack, life is so hard feat Hard Mad, kuwa na athma, Hip hop neno la uzima, mrs Azma feat Hard mad, chemsha bongo, nia moja feat Rado, we never give up feat Dark Master n.k.
Kwa sasa Azma yuko jijini Dar es salaam akiendelea kuuza album yake ya awali ya Love stories akiwa chini ya usimamizi wa Tamadunimuzik.

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment