
‘Deport Bieber Petition’ iliyoandikwa kwenda kwa Rais Barack Obama
kuomba Bieber arudishwe kwao inasema kuwa, watu wa Marekani wanahisi
wanawakilishwa kimakosa katika ulimwengu wa utamaduni wa Pop, hivyo
wanaiomba serikali imrudishe kwao Bieber.
Inaendelea kusema sio tu anahatarisha maisha ya vijana wa Marekani
lakini pia anawa influence vibaya vijana hao hivyo wanaomba Justin
Bieber aondolewe katika jamii yao.
“We the people of the United States feel that we are being wrongly
represented in the world of pop culture. We would like to see the
dangerous, reckless, destructive, and drug abusing, Justin Bieber
deported and his green card revoked. He is not only threatening the
safety of our people but he is also a terrible influence on our nations
youth. We the people would like to remove Justin Bieber from our
society.”
Hata hivyo Red light inaelekea kuwaka kwa msanii huyo sababu tayari ombi
hilo la kufukuzwa kwa Bieber limepata zaidi ya sahihi laki moja ambazo
huhitajika ili serikali itoe tamko rasmi juu ya ombi la kufukuzwa kwkae
nchini humo. Mpaka saa 2 na nusu usiku wa jana tayari zilikuwa
zimepatikana sahihi 100,633.
Bieber haishi nchini Marekani kwa Green Card ambayo humpa mtu ruhusa ya
makazi ya kudumu, bali anatumia Visa maalum ambayo hupewa watu maarufu
kama waigizaji, wanamuziki, wasomi au watu wengine wenye high profile
ambao serikali inaona ni wageni muhimu.
Hata hivyo mashabiki wa dhati wa Bieber wameonekana wakijaribu kumtetea
katika website ya Whitehouse, huku wakisema sio haki na hastahili
kufukuzwa. “With your help, we can stop it. He’s human. He’s not
perfect. The media sees the bad side of him. Please. He’s saved so many
lives. Including mine. A lifesaver, Shouldn’t deserve this.” Mmoja wa mashabiki hao aliandika.
Hata hivyo petition hiyo ya kumtetea haikufanikiwa kupata sahihi za kutosha, mpaka Jumatano asubuhi ilikuwa na sahihi 1,400 tu.
Serikali ya Marekani imeahidi kutoa majibu ya petition zinazofikisha
sahihi laki moja, japo inaweza kuchukua wiki, mwezi au hata miaka kupata
majibu ya serikali juu ya petitions zilizopo ikiwemo ya Bieber.
Source: Washington Times
0 comments:
Post a Comment