Dayna Nyange asema anasubiri jibu la COSOTA soon kumaliza kesi yake na Diamond.


Mwimbaji huyo wa ‘Nivute Kwako’ ameiambia Hot show ya Highlands fm kile kinachoendelea na kwamba bado swala hilo liko COSOTA na yeye anaendelea kusubiria majibu, lakini anapata mrejesho kidogo kuhusu kile kinachoendelea japokuwa haruhusiwi kuyaongea.
Hata hivyo Dayna ameonesha hali ya kuwa na mashaka kidogo kwa kile kinachoendelea kutokana na mrejesho anaoupata, japokuwa hakuzungumza nini hasa kinampa kigugumizi, lakini sentensi zake zinatoa picha.
“Mambo yetu yamekuwa na process kidogo, japo si kubwa sana, lakini tuombe Mungu..Mungu anaweza akajaalia muda wowote tukafikia muafaka, kwa sababu kwa upande wangu ninachosubiri ni maelezo tu, niitwe labda niambiwe kuna hiki na hiki.” Amesema Dayna.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment