WAKENYA WAMZOMEA MR. NCE NA KUMUITA MAC MUGA''SOMA KILICHOMKUTA
Msanii Mr Nice, amejikuta akizomewa na umati wa watu waliokuwa katika Club moja inayoitwa I club, ambapo wachekeshaji Fred Omondi na Mc Antonio hufanya show zao pale kila siku za jumapili.
Inasemekana Mr Nice alikua ameenda pale kwa ajili ya kula good time tu, na kufurahisha nafsi yake, lakini matokeo yake hayakua kama alivyotarajia. pale mchekeshaji Mc Antonio alipomuona Mr Nice katikati ya watu, na kwakuwa ni mtu maarufu, Mc akamuambia awapungie mikono watu waliokuwepo pale, lakini Mr Nice hakufanya hivyo wala kusimama akidai kuwa yeye ni msanii ambae amesainiwa na Mc huyo hawezi kumlipa yeye, na akipanda jukwaani hapo atashitakiwa na management yake.
Baada ya kusikia hivyo mashabiki walipata kichekesho kipya pale ambapo Mr Nice aliponyanyuka na kusema " Hamnilipi mimi nikipanda hapa kwenye jukwaa, nitashtakiwa mimi" baada ya kusema maneno hayo mashabiki walianza kumzomea huku wakipiga kelele wakisema Mac "Muga" wimbo wa Ally Kiba, ambao unasemekana kuwa unamdiss yeye. na dj hakuwa na hiyana aliupiga wimbo huo maana mashabiki waliutaka.Kwa hivi sasa Mr Nice ambae amehamishia makazi yake nchini humo yupo chini ya record label ya GRANDPA RECORDS ambapo yupo na wasanii wengine kama DNA na crew nzima ya KIDZ ambayo ni muunganiko wa wasanii wa label hiyo...
0 comments:
Post a Comment