KAMA WEWE NI MSANII HII INAKUHUSU: HIKI NDICHO ALICHOKUTANA NACHO NASH MC KUHUSU SANAA YA MUZIKI ALIPOHUDHURIA KIKAO CHA BUNGE DODOMA

Siku ya Jumatatu msanii Nash Mc Palestina alipata bahati ya kuhudhuria kikao cha bunge mjini Dodoma na hiki ndicho alichokiandika kwenye ukurasa wake wa facebook
NA HAYA NDIO MAMBO YA DODOMA,BAADA YA KUHUDHURIA KIKAO CHA BUNGE JUZI JUMATATU,NA SIKU HIYO PIA NILIFANYA KAZI KATIKA STUDIO ZA AFTER HISTORY NA MTAYARISHAJI WA KUITWA,DOUBLE!! KWA KWELI KWA JINSI NILIVYOISIKILIZA NA KUIELEWA HOJA YA BAJETI KUTOKA WIZARA YA HABARI,VIJANA,MICHEZO NA UTAMADUNI ILIYOSOMWA NA WAZIRI MWENYE DHAMANA KATIKA WIZARA HIYO,KWA UPEO WANGU MDOGO,NI WAZI SERIKALI HAINA MPANGO WOWOTE WA KUWASAIDIA WASANII WA TASNIA ZOTE KULINGANA NA MAELEZO YA BAJETI YAO,NA HILI LILIWEKWA WAZI NA MBUNGE NYAMBARI NYANGWINE KWA KUSEMA KAULI YA DHARAU KWA WASANII ETI,YEYE ANATAMBUA WASANII AU MSANII NI YULE MUANDISHI WA VITABU TU. KWA KAULI KAMA HIZO WASANII WENZANGU KAENI MKIJUA KUA SERIKALI HAIPO NA SISI,NA HAINA MUDA WA KUPAMBANA NA HUO UNAOITWA UHARAMIA SIJUI UPUUZI GANI, NDIO MAANA TAMADUNIMUZIK TUNASAMBAZA WENYEWE KAZI ZETU NA KUBUNI VITU KAMA KILINGE!NASAHA ZANGU KWAKO MSANII,PIGANA,PAMBANA HAKIKISHA UNASIMAMA MWENYEWE IWE KWA SHIDA AU KWA RAHA!!NAWASHUKURU VINEGA KWA KUNIPA MUALIKO NA HAYA NDIO MAWAZO YANGU.KWA MUNGU KILA JAMBO LINAWEZEKANA! MWENYEZI MUNGU TUBARIKI!!!
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment