Hivi karibuni rappers wanaoheshimika kwa uandishi mahiri wa mashairi,
One the Incredible na Nikki Mbishi wameonekana wakichill na Lady Jaydee
pamoja na kuchat mara kwa mara kwenye Twitter kitendo kinachoashiria
kuwepo uhusiano wa karibu baina ya wasanii hao.
One amesema anamchukulia Lady Jaydee kama dada ambaye amelea wasanii wengi kwenye muziki wa Tanzania.
“Sisi tupo karibu naye sababu ni sister, anatupaga mawaidha mawili
matatu. Watu wamesahau kwamba mimi video ya black on black tulifanyiaga
Nyumbani Lounge muda mrefu mbona. Au watu wengi hawajui kwamba Jide
alianzaga kuchana kabla hajaanza kuimba, watu wengi wameanza kumfuatilia
Jide wakati anaimba hawajui kwamba Jide alikuwaga mchanaji vile vile.
Ni support tu, it’s just love sababu tunaweza tukalink na watu tofauti
na wanaonesha na nini…. na sisi ni new artists so it’s very good, ni
support nzuri,”
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment