LAURYN HILL AENDA JELA KWA KUKWEPA KULIPA KODI


Mwanadada mkongwe kwenye muziki, LAURYN HILL (37) amehukumiwa kwenda jela kwa muda usiopungua miezi mitatu ...
LAURYN HILL ambae alikuwa katika kundi la muziki lililowahi kutamba sana miaka ya 90, FUGEES alikuwa mahakamani siku ya jana (Jumatatu) na hakimu kumuhukumu kifungo hicho kwa ukwepaji wa KODI uliofikia dola za kimarekani $1.8 millioni ...

Pamoja na kifungo hicho, LAURYN ameongezewa kifungo kingine cha ndani ambacho atafungiwa kifaa maalumu cha kumuangalia ambacho mara nyingi hufungwa mguuni ...

Wakati wa hukumu, Ms. LAURYN HILL alijitetea kuwa alikuwa anataka kulipaKODI hiyo lakini alishindwa kwa sababu za kimuziki ambao hafanyi vizuri kwa sasa kibiashara na alikuwa akilinda watoto wake ...
Ms. HILL anatakiwa kuripoti gerezani Tarehe 8 mwezi wa 7 kuanza kutumikia kifungo chake ...
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment