Wanamuziki maarufu kutoka Nchi jirani ya Uganda wanaojulikana kama Radio & Weasel wamechaguliwa kuwania tuzo za BET Awards 2013 ambazo zinatarajia kufanyika mwishoni mwa mwezi ujao, June 30 mwaka huu.
Wasanii hao wamechaguliwa katika kipengele cha Best International Act: Africa, ambapo ndani ya kipengele hicho wasanii wengine waliochaguliwa ni 2Face Idibia (Nigeria), Toya Delazy (South Africa), Donald (South Africa), Ice Prince (Nigeria), R2Bees (Ghana) pamoja na Radio and Weasel (Uganda).
Pia imeelezwa kuwa rapper Drake ndiye msanii pekee aliyekuwa nominated kwenye vipengele vingi kuwania Tuzo hizo za BET ambapo hadi sasa rapper Drizzy ametajwa kuwania jumla ya Tuzo 12, akifuatiwa na KendriCk Lamar pamoja na 2Chainz wote wakiingia kwenye kinyang'anyiro hicho kwenye categories 8, akifuatiwa na A$AP Rocky kuchaguliwa mara 5 ,Miguel mara 4, Rihanna,Justine Timberlake na Kanye West wamechaguliwa mara 3.
0 comments:
Post a Comment