Alichokifanya FID Q katika kumuenzi Bi Kidude


Kuna uthubutu wa kusema kuwa hili inawezekana kuwa ni wazo zuri na jema kabisa ambalo toka mwaka uanze umewahi kulisikia ...
Rapper kutoka ROCK CITY, Fid Q amependekeza kujengwa kwa kumbukumbu itakayomuenzi ambayo pia itatumika kusaidia waliokuwa karibu na marehemu Bi. Kidude aliyefariki na kuzikwa jana huko visiwani Unguja ...
Fid Q amependekeza kufanyika kwa jambo hilo hata kwa harambee itakayochangisha fedha za kufanikisha kitu hicho ...
Kwa kuanzia, Fid Q ambae alipata nafasi ya kurekodi wimbo pamoja na marehemu,"JUHUDI ZA WASIOJIWEZA" uliokuwa kwenye album yake ya Propagandaametoa mauzo yote ya miito ya simu, yaani Ring Back Tones [RBT]yatakayouzwa kwa wananchi na wapenzi wa muziki katika kusaidia ujenzi wa museum hiyo ...
Fid Q "Sitachukua hata thumni ..."
Hiki ni kitu cha kujivunia kuwa na mwanamuziki kama huyu ambae naweza kusema anauona umuhimu wa wanamuziki wakubwa hapa nchini, Bi. Kidude amekuwa mwanamuziki wa Taarabu aliyefanya vizuri sana na kuitangaza nchi hii ...

R.I.P Bi. Fatuma binti Baraka a.k.a Bi. Kidude

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment