#BreakingNews Baraza la sanaa Tanzania [BASATA] limemfungia msanii
Wa Bongo Fleva Shilole kutojihusisha na kazi yoyote ya sanaa kwa muda
wa mwaka mmoja.
Barua kutoka BASATA Inasema
“9 May 2015 ukiwa katika onyesho lako la
muziki Ubelgiji ulicheza uchi mbele ya hadhira ya wapenda sanaa za
Tanzania hivyo kudhalilisha utu wako na jamii ya kitanzania kimaadili,
BASATA ilipata habari zako, kumbuka pia October 2013 BASATA lilikuonya
na ukakiri kwa kuomba msamaha tabia yako ya kucheza bila kuzingatia
maadili uwapo jukwaani, BASATA ilikupa nafasi ya kutoa maelezo kwanini
usichukuliwe hatua za kinidhamu kwa kitendo chako lakini umekaidi kutoa
maelezo yako ” Inaendelea hapa
“Baraza limejiridhisha kwamba ulikiuka
maadili ya kazi ya sanaa kwenye onyesho lako huko Ubelgiji makusudi na
umekiuka sheria kwenye ibara ya 30 (2) ya katiba ya jamuhuri ya muungano
wa Tanzania ya mwaka 1977 kwa kuvunja maadili ya jamii ya Mtanzania
hivyo baraza linakusimamisha kujishughulisha na kazi za sanaa nchini na
nje ya nchi kwa mwaka mmoja, kufanya kinyume na hayo kutapelekea kupewa
adhabu zaidi pamoja na yeyote utakaeshirikiana nae”
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)


0 comments:
Post a Comment