Toka lianze seke seke la ugomvi baina ya wawili hawa Lil wayne na Bird man wa Ymcmb,habari zimezidi kuwa nyingi kwenye mitandao kila kukicha juu ya suala la Wayne kucheleweshewa kwa album yake ya 'the carter v"
Kwa mujibu wa mtandao wa tmz,Weezy ameripoti kuwa ikiwa Bird man atarudisha hela zake zote anazomdai basi yeye yupo tayari kurudi Cash money kama zamani lakini sio kwa asilimia zote.
Wayne alisema kuna malipo mawili ambayo yanatakiwa kuwepo ikiwemo dolla millioni nane $8,000,000 pamoja na dolla millioni mbili zilizotumika kukamilisha album yake mwezi uliopita.Imeripotiwa kuwa endapo Lil wayne atalipwa dolla millioni kumi $10,000,000, hatokuwa na kipingamizi ingawa alisha sign mkataba wa dolla millioni hamsini namoja. $51,000,000 kwasababu alitegemea atapata faida kwenye siku zijazo.
0 comments:
Post a Comment