Msanii Nikki wa Pili kutoka katika kundi la muziki wa Hip hop Weusi
ambao masikani yao ni jijini Arusha ameweka wazi kuwa siku za karibuni
itafahamika hatima ya Msanii Lord Eyes ambaye awali alilipotiwa
kuondolewa katika kundi hilo,Nikki aliweka wazi hilo alipokuwa akichat
Live katika ukurasa wa Facebook wa EATV katika kipengele cha
Kikaangoni Live kinachokukutanisha na mtu maarufu
Moja ya maswali ambayo yameeulizwa sana na mashabiki kwa Nikki wa Pili
ni kuhusu hatima ya msaniii Lord Eyes ambae alitimuliwa katika kundi
hilo,hivyo msemaji wa weusi kampuni Nikki wa Pili akafunguka na kusema
kuwa siku za karibuni msaniii huyo atarudi Weusi na kuendeleza harakati
za muziki kwani amedai kuwa weusi ni kampuni inayoundwa na watu watano
kwa mujibu wa sheria akiwemo Lord Eyes.
"Lord Eyes soon atarudi weusi maana sisi kama weusi kwa pamoja ni
kampuni,hivyo weusi ni mtu 5 kama memorandam ya kampuni inavyo sema"
mbali na kuzungumzia kundi na hatima ya Lord Eyes Nikki amefungua siri
nyingine kuwa kuna ngoma nyingine wamefanya na mwanamuziki bora wa Hip
Hop kwa mwaka 2014 ambaye ni Fid Q na kudai kuwa kazi hiyo mpaka sasa
bado hawajaitambulisha na waliifanya toka mwaka jana hivyo wakati
utakapofika wataitoa ngoma hiyo.
Akiweka wazi mipango ya weusi kutoka Nikki amedai kuwa baada ya yeye
kutambulisha na kupokelewa vizuri na ngoma ya sitaki kazi,wimbo mwingine
utakaofuata utakuwa wa mkali Joh Makini.
Nikki wa pili akuacha kutoa somo kwa baadhi ya wasanii wa bongo ambao
wamekuwa wakiipuuza Elimu na kukimbilia kufanya muziki na ujumbe wake
kwao ni kuwa Elimu haina mbadala na kusoma ni kuchagua kuishi ukiwa na
uhuru na ishara ya kustarabika katika jamii.
"Elimu haina mbadala...kusoma ni kuchaguwa kuishi huru na ku staarabika"
MSANII ANAEMKUBALI Nikki wa Pili amesema kuwa katika maisha yake yote
amekuwa akitamani namna Jay Z alivyoishi maana alitoka katika maisha
magumu na kubadili maisha yake hayo na kuwa mfano wa kuigwa katika mambo
mengi,na amesababisha watu wengi kuamini kuwa historia ya maisha yao
haiwafanyi kushindwa maisha.
"Namkubali sana Jay z..kaipeleka hip hop ikulu, na katika level za
juu kibiashara,,pia ametuaminisha tulio kulia katika umaskini kuwa
unaweza kuwa mtu yoyote historia yako haijalishi"
Nikki wa Pili ni msanii ambae kwa sasa anatamba na wimbo wake wa sitaki
kazi,ambao ameamua kuihamasisha jamii hususani vijana kuacha dhana ya
kutaka kuajiriwa bali wanaweza wenyewe kutafuta njia nyingine na kuweza
kujiajiri wenyewe na kutengeneza ajira kwa watu wengine jambo ambalo
baadae linaweza kuja zalisha mahitaji makubwa ya kazi
Home / Uncategories / Nikki wa II aeleza kuwa wapo kwenye harakati za kumrudisha Lord Eyes ndani ya kampuni ya WEUSI
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)

0 comments:
Post a Comment