MB Dog aliwahi kulipwa shilingi Milioni kumi kwa show moja miaka ile


Kama ulifikiri bongo fleva ilianza kulipa mamilioni miaka ya akina Diamond Platinumz, Ommy Dimpoz na wengine, nikimaanisha kuanzia mwaka ya 2010, kwa leo inabidi ubadili mawazo yako.
“Lakini uzuri wakati mimi naanza kufanya, kazi zilifanyika na misingi za ile kazi zilikuwa zimekaa tofauti na watu wanavyosikia. Kwa hiyo uoga hata wa mapromota ulikuwepo wakati wanatusogelea. Kwa hiyo hatukuwa tunalipwa laki tatu viiile.” Mbwana Mohammed aka MB Dog ameiambia HOT SHOW YA Highlands Fm.
Huenda inawezekana ulikuwa hujui kwa sababu wakongwe waliokuwa wanahit enzi hizo hawakuwa na tabia ya kuweka wazi kiasi wanacholipwa kama wanavyofanya wakali wa bongo flava wa kizazi hiki cha dijiti.
Mkali huyo wa ‘Latifa’ ameiambia Highlands  Fm kuwa alikuwa anakutana na milioni kadhaa kwenye show zake, na kwamba kiasi kikubwa zaidi alichowahi kulipwa kilikuwa shilingi milioni kumi nchini Burundi.
“Yaani mimi show ya kwanza nimeanza kuifanya nimelipwa milioni tatu, show ya mwisho mimi kuifanya nimelipwa milioni kumi...ambayo ndiyo ilikuwa show ya maajabu yaani...kwa ubongo wangu  nawaza naweza kufanya show tena ya watu wengi kama wale!! Nadhani ilikuwa mwaka 2006.” Amesema MB Dog na kusisitiza, “milioni kumi za kitanzania”.
Kumbe Bongo Flava ilianza kulipa zamani japo kwa wachache! Na huenda ni kwa sababu tu watu walikuwa hawaweki wazi wanachoingiza.
Hapa tumpigie picha Mr. Nice wa enzi hizo kwa kutumia mfano wa MB Dog.
Kama kweli mambo yalikuwa hivi, inaweza kuwa moja kati ya sababu zilizozaa wazo kati ya wakongwe Juma Nature na Lady Jay Dee kutaka Leo iwe ‘Kama Jana
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment