ABDUL KIBA AZUNGUMZIA SABABU ZA KAKA YAKE ALLY KUWA KIMYA KWENYE GAME

 
Ali Kiba, mwimbaji aliyewahi hutajwa na mfalme wa R&B duniani Robert Kelly kama mmoja kati wa wasanii wenye sauti poa zaidi katika mradi wa One 8 amekuwa kimya kwa kipindi cha mwaka mmoja, huku wengi wakitoa sababu kadhaa za kufikirika kuhusu ukimya wake.
  STREET CONSCIOUS imeongea na ndugu wa damu wa Ali Kiba, Abdul Kiba ambaye mbali na kuwa msanii aliyetambulishwa kwenye game na kaka yake, amekuwa akisaidia kuzifuatilia na kuzisimamia kazi zake.
Abdu Kiba ameeleza kuwa ukimya wa ndugu yake unatokana na kubanwa na majukumu ya kifamilia.
“Unajua watu wengi wanahisi vibaya sana, mara mwingine anaibuka na kusema amefulia kwenye game,sio kweli naomba niweke sawa kuhusu suala hili ni kwamba Ally Kiba alikuwa na majukumu ya kifamilia pamoja na kazi zake,maana nakumbuka tangu anitambulishe kwenye muziki wa Bongo Flava ndio alianza kubanwa na mambo  yake binafsi.” Amesema Abdu Kiba.
Hata hivyo, mashabiki wa Ali Kiba wana kila sababu ya kukaa mkao wa kusikia hits za mkali huyo mwaka huu.
“Niliwahi kuzungumza nae hivi karibuni, akaniambia mwaka huu anatarajia kuja kivingine katika game. Kwa sasa anajaribu kumalizia baadhi ya nyimbo alizorekodi ili mwaka huu mashabiki wazisikie katika vituo mbalimbali vya radio.” Abdu Kiba aliieleza
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment