Rapper wa Detroit Eminem anatarajia kushika nafasi ya pili mwaka 2013 kwa kuwa na albam iliyouza zaidi kwenye wiki ya kwanza. Kwa mujibu wa Billboard, albam ya nane ya Eminem, The Marshall Mathers LP 2 ipo mbioni kukamata nafasi ya kwanza kwenye chart ya Billboard 200 kwa kuuza kopi 700,000-750,000 kwenye wiki ya kwanza.
Albam hiyo itakuwa ya saba Mfululizo kushika namba moja. Ni albam yake ya 1999, The Slim Shady LP tu ndio ambayo haikuingia kwenye top 10. Namba hizo zitaifanya albam ya Slim Shady kuuza kopi nyingi zaidi mwaka huu nyuma ya albam Justin Timberlake, The 20/20 Experience, iliyouza kopi 968,000 mwezi March.
Kwa sasa Drake anakamata nafasi ya pili ambapo albam yake ‘Nothing Was the Same’ iliuza kopi 658,000, Sept 1 katika wiki yake ya kwanza.
0 comments:
Post a Comment