Mariah Carey adai kazi ya ujaji wa American Idol, ilikuwa kama kufanya kazi na ‘shetani jehanamu’


Mariah Carey amefunguka kwenye interview na Angie Martinez wa Hot 97 Jumanne hii na kuelezea jinsi alivyojisikia kufanya kazi ya ujaji wa shindano la American Idol.
“Ukweli niliichukia,” alisema. “Hivi ndivyo ilivyokuwa. Nilikuwa mtu wa kwanza kusainiwa.. nilidhani litakuwa jopo la watu watatu. Walinipa pesa nzuri, na nilisema ‘Sawa, Randy Jackson atakuwepo, nimemfahamu kipindi chote, alikuwa akinipiga gitaa la besi. Hakuna kitu kigumu.’”
“Lakini haikuwa hivyo. Ilikuwa ni kama kwenda kazini kila siku jehanamu kufanya kazi na shetani.”
Carey hakuweka wazi ni jaji gani mwezake aliyekuwa kama shetani, lakini hakuna siri kuwa alikuwa akilumbana na Nicki Minaj kwenye msimu wote. Wawili hao walikuwa wakijikuta wakirushiana maneno wakati wa usaili na ugomvi wao kuupeleka mtandaoni mara kadhaa.
Mariah ambaye ni mama wa watoto wawili, amerejea tena studio kuendelea na muziki. Yeye na Nicki hawatarejea tena kama majaji kwenye msimu wa 15 wa American Idol.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment