JAY Z KUZINDUA PERFUME YAKE





RAPPER Jay Z ameendelea kuonesha kuwa yeye ni mjasiriamali baada ya kufungua miladi mbalimbali ikiwemo kuanzisha perfume za kiume alizozipa jina la 'Gold'.

Kutokana na hilo rapa huyo amejiweka katika nafasi nzuri ya kuendelea kuingiza pesa nyingi kupitia mradi huo na biashara zake nyingine.

Perfume hizo zinatarajiwa kuzinduliwa November 20, mwaka huu huku bei yake ikitarajiwa kuwa ni $70, ambapo perfume hizo zinapatikana katika chupa tatu.

Ili kuongeza ubora wa Perfume hizo ameweka wazi uwa anampango wa kuongeza deodorant pamoja na shower gel zitakazoongeza mvuto na manukato ya perfume hizo.

Kutokana na hilo Jay Z anazidi kudhihirisha kuwa hakufanya makosa kukamata nafasi ya pili katika orodha ya jarida la Fobres ya wasanii wa Hip Hop waliotengeneza fedha zaidi kwa kuingiza dola milioni 43 kupitia kazi zake za muziki na biashara mbalimbali anazomiliki.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment