Haya Ndiyo Mafanikio Ya Cindy Rulz Tangu Aanze Muziki …

streetconscious.blog


Rapper Cindy Rulz anazidi kufanya vizuri katika soko la buridani hapa nchini na Nchi za nje, na hii ni kutokana na muziki wake kuzidi kusambaa katika wigo wa kimataifa sasa, sio Afrika tu. Uwezo wake wa kuchana kwa lugha mbili tofauti yani Kingereza na Kiswahili unamnyooshea wigo rappee huyo pia.
Ngoma ya Lets Wait aliyoichia hivi karibuni ni wimbo mzuri sana kiasi cha kufanya baadhi ya mashabiki wa Cindy Rulz kuhisi kuwa huo ni wimbo mkali kuliko zote alizowahi kufanya. Pongezi liende kwa Producers, Lamar na Dunga ambao kwa kiasi kikubwa pia wamefanya wimbo huo kufika levels iliyopo sasa.
Pia Lyrics za wimbo huo zimekuwa certified na Rapgenius, kwa maana hiyo mashairi ya wimbo huo yanapatikana kwenye website kubwa ya mashairi nchini Marekani, Rapgenius.com ambayo inatembelewa na mamilioni ya watu kila siku.
Mtu wa kwanza hapa Bongo kusikia akiwa amewekewa mashairi kwenye mtandao huo ni Gosby, sasa Cindy Rulz naye amefanikiwa kufikia huko. Kwa sasa watu kutoka sehemu mbalimbali duniani wanaweza kusoma mashairi ya Lets Wait na kusikiliza wimbo huo kwa wakati mmoja.
Pia mwanadada Cindy hakuishia hapo kwani siku chache baada ya kurelease wimbo huo mpya akaachia video ya wimbo wake uliopita, Utanifanya Nighairi ambao amemshirikisha Chidy Bway, ngoma hii ameifanyia G. Records kwa KGT.
Kitu kizuri kuhusu hii video ni jinsi ilivyopokelewa vizuri na mashabiki wa muziki wa Bongo Flava. Lakini kizuri zaidi ni pale mtandao mkubwa wa Marekani tena viewhiphop.com kuupromote au kuupa shavu kwa kuitupia video hiyo kwenye mtandao wao.
Haya ni mafanikio ambayo wasanii wengi wa Bongo hawayapati na matokeo yake wanaishia kusikika hapa hapa nyumbani. Mafanikio haya pia yanarahisisha collabo na wasanii wakubwa duniani  na pia kupatikana kwa nafasi ya kusikika na watu wa nchi nyingine na kuufanya muziki kukua zaidi.

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment