Rapper toka Bongo CORRINE MARY a.k.a CINDY RULZ ametoa pongezi na shukurani zake za dhati kwa wasanii wenzake wa kike ambao humpa ushirikiano kwa kuzisambaza nyimbo zake mpya mara kwa mara katika mitandao ya kijamii na media mbalimbali.
Akipiga Stori na kipengele cha Chumba Cha Sindano kupitia kipindi cha Kali za Bomba hapa Bomba FM Mbeya, hitmaker huyo wa Unstoppable, Party ya Cindy na Lets wait CINDY RULZ amesema licha ya muziki wa hiphop bongo kuwa na wadau wachache wanaousapoti lakini anatambua fika haitochukua muda muziki huo kuteka mashabiki wengi kutokana na kufuata misingi.
“Sasa hivi nachoshukuru Mungu ni kwamba wako more supportive wote female rappers ambao nawafahamu kawa wapo CHIKU K kuna DIVAwote tumekuwa response, maana nakumbuka hata nilipotoa hii Cover, isitoshe ali-post kwenye mitandao yake ya kijamii, CHIKU K alikuwa anaandika Status yaani ndo iko hivyo. Kwa sasa hivi tupo pamoja zaidi tunaandaa kitu kwa pamoja wote sisi sote wanne kwa hiyo siwezi kusema ni competition zaidi tunajitahidi kujisukuma sisi wenyewe ka wenyewe, lakini ukiangalia hao wengine sijui wanaoimba RNB nini naweza nikasema kwamba it nice wameanza kueleweka zaidi kuliko sisi na sisi ndiko tunakoelekea” alisema CINDY RULZ
Kwa hatua nyingine Rapper CINDY RULZ ameweza kuelezea mikakati na ahadi alizopewa baada ya ngoma ya Lets Wait aliyomshirikisha DUNGAkuwekwa kwenye tovuti ya kimataifa www.hotnewhiphop.com na blogs mbili za Dearth Chambers na Grime Culture na kueleza furaha yake “(Anaanza kwa kucheka) kwanza sikutegemea kabisa kwa sababu unajua na-rap kwa Kiswahili kwa hiyo ni tofauti kwa huko kuweza kuelewa hiyo lugha, lakini nacho shukuru Mungu ndo hivyo walinitumia email wakasema wamependa quality ya nyimbo hata kama wao walikuwa wao walikuwa hawaelewi naongea nini, lakini delivery yangu iliwafurahisha niweze kusema kwa hiyo wakasema watakuwa wananisapoti niendelee kutuma nyimbo zangu huko”.
WWW.STREETCONSCIOUS.BLOGSPOT.COM
0 comments:
Post a Comment