:Rado asema uhusiano mbaya ni chanzo cha baadhi ya wakongwe kupotea


Rapper Rado toka Mwanza ambae kwa kipindi kirefu amekuwa nje ya game la bongo hasa ‘Main stream’ amesema kuwa uhusiano mbaya kati ya wadau wa muziki na wasanii wakongwe ni chanzo cha baadhi ya wasanii wakongwe kupotea katika game.Rado alisema mengi alipokuwa akihojiwa kwa njia ya simu na kipindi cha Hot Show katika redio Highlands fm jijini mbeya alisema:
“Mi nachoweza kusema wazi kuwa tatizo ni kuwepo uhusiano mbaya kati ya wadau wa muziki na wasanii wakongwe, uhusiano huo umeharibiwa zaidi kutokana na watu kufanya hii sanaa ku-base katika masilahi binafsi, kwa sababu unakuta wadau wanajua wasanii wa muda mrefu wana taarifa nyingi kwa hiyo huwezi kumpanga kila siku. Kwa sababu bahati mbaya kumekuwa hakuna hilo, mpaka uwe una mtu ndo ueleweke.” Amesema Rado aka Uso.
 “Hakuna ile misingi halisi, kwenye hip hop tunaita element, na hii inasababisha wasanii hata wa muda mrefu washindwe kulalamika,” ameongeza Rado.
Akizungumzia kuhusu uhusiano wake kwa sasa na Fid Q ambae hawakuwa na uhusiano mzuri miaka mingi iliyopita, Rado amesema hakuwahi kuwasiliana nae tangu alipoachia ‘Usiulize’.
“Hatukuwasiliana kabisa, na hii inatokana na content zilizokuwepo, mwanzoni tulikuwa tunawasiliana zaidi kuliko baada, hatukuwa tena na mawasiliano kwa sababu tayari yeye ana content nyingine, na mimi nina content nyingine.” Rado anaeleza.
Rapper huyo ambae wiki hii ameachia wimbo wa pamoja akiwa na Azma unaoitwa ‘Nia Moja’, amesema kwa sasa anafanya project iliyobeba harakati alizozipa jina ‘Chemichemi na Wana’ itakayohusisha wasanii wengi zaidi nchini.
Rado ameiambia HOT SHOW kuwa ana wimbo mpya atakaoanza kuusambaza soon, na kwamba anafanya kazi na studio ya One Love FX ya jijini Mwanza
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment