Mr Blue Aelezea sababu za Yeye kutoonekana kwenye Video Ya Hemedy- Rest Of My Life


 
 Mr Blue ameeleza Kuhusu sababu za kupotezea video ya Hemedy Phd - Rest Of My Life iliyotoka Ijumaa. 

Blue amesema "Ni kweli Hemedy alinitafuta tufanye video ila wakati huo nilikuwa na show nje ya nchi na nilivyo rudi sikuwa na nafasi ila tulikubaliana kuwa tuta shoot hivi karibuni, Blue amendelea kusema  Ameshangaa sana kusikia kuwa video imetoka bila yeye kuwepo na kuwa Hemedy amechana mistari yake, Sina sababu ya kutokuwepo kwenye video ya Hemedy kwani sisi ni marafiki na nampa heshima sana Hemedy kama kaka yangu, Nikimuona Hemedy nitamuliza kwanini ameshindwa kusubiri mpaka niwe na muda wa kufanya sehemu yangu na ametoa video bila mimi"

Mr Blue Alimaliza kwa kusema kuwa Atakacho fanya ni kumtafuta na wayamalize na kama kutakuwa na version ya pili ya hii video basi anauhakika wa kuwepo kwenye kipande chake alisema.

Baada ya kuongea na Hemedy na Mr Blue nimegundua kuwa hawana maelewano mazuri hawa wasanii wawili kwa sababu hakuna mwenye maelezo kamili ya issue hii na pia hapa Tanzania hakuna msanii mwenye sababu ya msingi ya kuto onekana kwenye video ya mwenzake unless anataka kuharibu kazi ya Mwenzake au wamegombana.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment