Juzi albam ya Jay-Z Magna Carta Holy Grail ilikamata nafasi ya kwanza kwenye chart za Uingereza. Jay-Z hajawahi kukamata zaidi ya No. 4 kwenye chart za mauzo ya juu ya nchini Uingereza ambapo albam yake ya mwaka 2009, Blueprint III iliwahi kushika namba nne.
Lakini pia albam ya mwisho ya Jay-Z kuwa na mafanikio kiasi kama hayo ni Watch The Throne aliyokuwa na Kanye West, ambayo ilikamata nafasi ya tatu.
Kwenye chart za nyimbo moja moja, Blurred Lines ya Robin featuring Pharrell Williams na TI imekamata nafasi ya kwanza. Katika hatua nyingine Jay-Z alikuwa mmoja wa wasanii waliotumbuiza kwenye tamasha la Wireless music festival jijini London.
Rapper huyo aliperform wimbo ‘Holy Grail’ na Justine Timberlake lakini pia Rihanna alitumbuiza naye baada ya kupanda kwa surprise.
0 comments:
Post a Comment