Profesa J akiwa na mama yake mzazi Bi Rosemary Majanjara Haule enzi za uhai wake. Picha hii ilipigwa April 4, 2008 katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam wakati wa sherehe ya uzinduzi wa albamu mpya ya Profesa J ya 'Aluta Continua'
HABARI ZILIZOPOKEWA USIKU HUU NI KWAMBA MAMA YAKE MZAZI MSANII MAARUFU WA MUZIKI NCHINI, JOSEPH HAULE A.KA. 'PROFESA J' AMEFARIKI DUNIA USIKU HUU BAADA YA KUGONGWA NA GARI MAENEO YA MBEZI JUU, JIJINI DAR ES SALAAM, ALIKOKUWA ANAISHI NA MWANAE.
HABARI ZINASEMA MAREHEMU, BI. ROSEMARY MAJANJARA HAULE, ALIGONGWA NA GARI AKIWA ANAVUKA BARABARA KUELEKEA DUKANI KIASI CHA SAA MBILI USIKU, NA KWAMBA BAADA YA KUGONGWA WASAMARIA WEMA WALIMKIBIZA HOSPITALINI TUMBI KWA KUTUMIA BAJAJI AMBAKO ALIFARIKI DUNIA. TAARIFA ZA AWALI HAZIJATAJA AINA YA GARI NA KAMA BAADA YA AJALI HIYO LILISIMAMA AU LA.
PROFESA J AMETHIBITISHA HILO MUDA MFUPI ULIOPITA, NA KUSEMA INAMUIA VIGUMU KUAMINI IMETOKEA KWANI ANASEMA MAREHEMU MNAMO SAA MBILI HIVI ALIMPIGIA SIMU NA KUMWELEZA KUWA AMEPATA AJALI NA KWAMBA WAKATI HUO YUKO KITUO CHA POLISI, BILA SHAKA KUPATA FOMU YA PF 3 YA KUMUWEZESHA KWENDA KUTIBIWA HOSPITALI.
"MAMA ALINIAMBIA MWANANGU NIMEGONGWA NA GARI....NJOO NIKO POLISI NAANDIKISHA....MWANANGU NAKUFA....ALINIAMBIA MAMA NA MARA SIMU IKAKATIKA. KILA NILIPOJARIBU KUPIGA IKAWA HAIPATIKANI..." ALISEMA PROFESA J KWA UCHUNGU.
ANASEMA WAKATI ANAPIGIWA SIMU NA MAMA YAKE YEYE ALIKUWA KATIKA MGAHAWA WA NYUMBANI LOUNGE, NAMANGA, DAR ES SALAAM, ALIKOKUWA KATIKA KIKAO NA LADY JAY DEE NA MUMEWE GADNA G. HABASH, AMBAO BAADA YA TAARIFA HIYO WALIMSINDIKIZA HADI HOSPITALI YA TUMBI.
"TULIPOFIKA HOSPITALI SIKUAMINI KUONA BADALA YA KUPELEKWA WODINI AMBAKO NILIDHANI MAMA ATAKUWA AMELAZWA NIKAPELEKWA CHUMBA CHA MAITI AMBAKO NILIMKUTA MAMA AKIWA MAREHEMU", ALISEMA PROFESA J KWA MAJONZI.
GLOBU YA JAMII INATOA MKONO WA POLE KWA PROFESA J KWA MSIBA HUU MZITO NA WA KUSIKITISHA. TUNAMWOMBA MOLA AMPE NGUVU YEYE NA FAMILIA YAKE KATIKA WAKATI HUU MGUMU.
TUTAENDELEA KUWAPASHA KINACHOJIRI KADRI HABARI ZAIDI ZITAPOPATIKANA. KWA SASA PROFESA J NA WADAU WENGINE WAKO NYUMBANI KWAKE MBEZI JUU.
source-tzdailyeye
0 comments:
Post a Comment