HIVI NDIVYO SHOW YA LADY JAYDEE ILIVYOKUWA


 ONYESHO la mwanamuziki Judith Wambura Mbibo ‘Lady Jaydee’ kutimiza miaka 13 katika muziki, limefana usiku wa kuamkia leo katika eneo la maegesho ya magari kwenye ukumbi wa Nyumbani, Lounge, eneo la Kinondoni, Dar es Salaam kwa mamia kujitokeza kiasi cha kujaza eneo hilo, hadi kupishana ikawa taabu. Watoto wa mjini wanasema ilikuwa funika bovu- ndiyo shoo hiyo ilikuwa nzuri mno, ya kistaarabu, yenye mashamsham ya aina yake. 
Jide akikumbatiana na Profesa Jay


Jay akipagawisha


Jay akisema na nyomi
Wasanii nguli wa Hip hop waliomsindikiza Jadyee katika shoo hiyo, Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’, Joseph Haule na Juma Nature na kundi lake wanaume Halisi nao walifanya mambo mazuri jukwaani kiasi cha kuiongezea utamu shoo hiyo. Kufika saa 3:00 usiku tayari Machozi Band inayomilikiwa na Jide ilikuwa jukwaani kuanza kutumbuiza kabla ya kumpisha rapa Wakazi kutoka Ukonga, baadaye bendi ya M ikiongozwa na Grace Matata kwa shoo za utangulizi. Saa 5:00 usiku, Jide akapanda jukwaani na kuibua shangwe nzito kutoka kwa mamia waliokuwa wamefurika katika eneo hilo. Jaydee alianza na wimbo wa Nilishakuwaga na Wangu, baadaye akaimba Nakuhitaji, Moto, Mambo Bado, Yeye, Malaika, Siri Yangu, Wanock Nok kisha kumalizia na Single Boy katika awamu ya kwanza. Baada ya hapo, Jide akasema ilipotimu Saa 6:00 usiku ameingia katika mwaka mpya tangu azaliwe hivyo mashabiki wakamuimbia ‘Happy Birth Day’ kisha akateremka kwenda kukumbatiana na mama yake mzazi, Martha Mbibo na kumpa zawadi ya fedha zote alizokuwa ametuzwa jukwaani. Jide alirejea jukwaani na kuimba kwa ufupi nyimbo alizowahi kurekodi na wasanii Man Ngwair na Langa Kileo ambao hivi sasa ni marehemu, kabla ya kumpisha Mh. Mbunge wa Mbeya Mjini, Sugu ambaye aliimba nyimbo tatu tu, lakini alisisimua mashabiki ile mbaya. Sugu alianza na Hakuna Matata akimshirikisha Mkoloni, Sugu na kumalizia na Mambo ya Fedha ambao ulimrejesha jukwaani Jide. Kutoka hapo, ikawadia zamu ya Wanaume Halisi kutoka Temeke, wakiongoza na Juma Kassim Kiroboto ‘Sir Nature’, ambao nao walifanya balaa vile vile na kuurusha umati ile mbaya.
Msanii M2 The P akizungumza jukwaani
 
KR Mulla


Sir Nature


Nature na Doro
Sinta akimpiga picha Nature
Wakati Nature anaimba, mpenzi wake wa zamani Christine Manongi ‘Sinta’ alikuwa bize kumpiga picha ‘mzee’ wake wa kitambo, kiasi cha mmoja wa viongozi wa kundi hilo, Kiboya kupora kipaza sauti na kutamka Baba Sinta akimtania Nature, jambo ambalo liliwafanya watu washangilie.    Nature kabla ya kuanza kuimba alimpandisha jukwaani msanii M 2 P aliyezushiwa kifo wakati akiwa amelazwa Afrika Kusini sambamba na Man Ngwair. MP alisalimia na kushukuru kwa dua za Watanzania wakati akiwa taabani wadini, kwani zimemponya na akatumia fursa hiyo kumuombea swahiba wake Ngwair apumzishwe kwa amani peponi. Ndipo Wanaume wakaanza vitu vyao, wakipiga nyimbo za Sonia, Hakuna Kulala, Mzee wa Busara, Ladhia, Haipotei, Dance With Me na Jimwage. 
Jaydee na mama yake



Jaydee akikusanya fedha alizotuzwa


Anaziweka kwenye boksi kabla ya kweneda kumpa mama yake. Alyeshika boksi ni King Kiboya


TK wa M Band...


Maeneo kama haya Mh Sugu huwa si mkali...anajua kutabasamu


Rapa kutoka Ukonga





Wanaume walipoondoka akaibuka msanii mcheza ngoma za asili huku akichezea nyoka, Mango Star ambaye aliwaacha watu midomo wazi pale alipokuwa akimnyonya nyoka upande wa kichwani. Akafuatia mkongwe Komando Hamza Kelele ambaye kwanza alimpandisha mkewe, Stella John Momose Cheyo jukwaani kumtambulisha, kisha akaimba nyimbo na Tumetulia. Ikawadia zamu ya Profesa Jay, ambaye aliimba Joto Hasira pamoja la Lady Jaydee, baadaye, Teja, Yahya na Joto tena. Jaydee akateremka na kumuacha Jay amalizie shoo naye akamalizia vizuri kwa nyimbo za Hapo Vipi, Nikusaidiaje na Kamili Gado. Watu kadhaa waliofika Nyumbani Lounge kushuhudia shoo hiyo walilazimia kugeuka na kuondoka kwa sababu ukumbi ulikuwa ‘umejaa na hakuna pa kukanyaga’. Kwa ujumla shoo hiyo ilipendeza, ilikuwa bab kubwa
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment