Msanii wa muziki wa Kizazi Kipya Toka Manzese Ney Wamitego amesema Nikki Mbishi na
wasanii wengi wachanga huwa wanajaribu kuwa-diss wasanii wakubwa kwa
lengo la kupata jina.
Ney alizungumza hayo pale alipoulizwa juu ya kitendo cha msanii Nikki Mbishi kutengeneza wimbo
unaoitwa Ney Wamitego, wimbo ambao unaonekana moja kwa moja
unamzungumzia Ney Wamitego kama mwanamke au mwanaume siyo.
Mwanzoni Ney alipoulizwa anachukuliaje
kitendo cha msanii huyo kuandika wimbo unaomzungumzia yeye, Ney alikataa
kuzugumza hilo huku akisema "Yaani kaka mimi nikiongea kitu tu mimi
nampa kick ile anayotaka yule dogo, mi sitakiwi kuongea kitu, yaani hiki
ndio kitu ambacho watu wa karibu wamekuja wameniambia this time huyu
amefanya hiki kwa sababu ya hiki, so dont talk anything"
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment