Ni kama mambo yanawaendea kombo wasanii wanaounda crew ya Cramp Mula toka Kenya ambao walifanya vizuri zaidi mwaka jana hadi kufikia ha2a ya kuwemo kwenye orodha ya wasanii waliochaguliwa kushindania tuzo za BET Marekani.Lakini hivi karibuni first lady wa kundi hilo ajulikanaye kama Miss Kairun aliondolewa kwenye kundi hilo kwa madai kwamba anakwenda nchini Marekani kusoma chuo mwezi wa nane.Lakini baadae mitandao mingi nchini humo iliandika kuwa alitolewa baada ya picha zake za utupu kuzagaa.Baada ya muda mchache walimuongeza member mpya ambae amechukua nafasi ya Miss Kairun ambae na mwanadada TIRI.Sasa habari mbaya ni kwamba member mwingine wa crew hiyo ajulikanaye kama TAIO TRIPPER ametangaza rasmi kujitoa na kufanya kazi zake kama solo artist.Je huu unaweza kuwa mwisho wa Camp Mula?Lakini siku ya leo first lady mpya wa kundi hilo TIRI ameachia ngoma yake mpya aliyomshirikisha K'COUS inayoitwa MASH UP.Lakini pia leo kundi hilo limeachia rasmi video ya wimbo ALL INwaliomshirikisha M Anifest.. .
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment