SNOOP LION AZUNGUMZIA KUHUSU KIFO CHA 2 PAC NA B.I.G

Mkali kutoka west coast the hip hop legend.. long time rapper ambae amebaki kwenye main stream toka alivyoanza muziki “murder was the case they gave me”.. Snoop Doggy kwa sasa anajiita Snoop Lion, Snoop anahisi yuko sawa kuanza kufanya reggae, anasema Dr. Dre na wasanii wengine wakali wako nyuma yake wakimpa support katika hilo na pia akasema sio kwamba anataka aende Jamaica kwa ajili tu kufanya biashara hapana anataka asaidie Wajamaica ili wafaidike na kile wanachokitengeneza.
Akiendelea kupiga stories Snoop alisema baada ya Tupac na Notorious B.I.G kufa ilibadilisha kabisa mwelekeo wa muziki wa hip hop ndipo wasanii wengine wanaofanya vizuri sasa hivi wakapata nafasi na mafanikio.
Akipiga stories na Power 105.1 The Breakfast Club, Snoop alisema B.I.G na Tupac wamefungua mipaka ya Hip Hop na imefika sehemu ambapo isingeweza kufikishwa na marapper waliopo sasa. “ Unajua nini”nimekutana na maongezi kama haya zaidi ya mara mbili au tatu na nafikia hitimisho” Kama Tupac na B.I.G wangekuwepo marappers wengi wasingefika walipo sasa, na hiyo sio kwamba si onyeshi heshima kwa wasanii waliopo sasa” ni kwamba njia ilifunguliwa na wasanii wengine wakapata nafasi. Usingeweza kabisa kukaribia alichokua anakifanya B.I.G na Tupac” alisema Snoop Doggy...
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment